Breaking


Tuesday, August 15, 2017

web design

Taarifa za habari kutoka kwa mashirika ya kibiashara zinasema Kampuni ya kimataifa ya magari ya teksi, Uber, itaunganisha oparesheni zake nchini China, na kampuni hasimu nchini humo Didi Chuxing.
Ripoti zinasema mpango huo utakaogharimu dola bilioni 35 huenda ukatangazwa baadaye leo.
Tangu Uber izindue oparesheni zake nchini China mwaka wa 2014, imekuwa ikikabiliwa na upinzani mkubwa katika harakati za kupata sehemu kubwa ya soko la Uchina.
Kulingana na Bloomberg mpango huo utakaogharimu dola bilioni 35 utaipa Uber China,kampuni ya mtandao ya Baidu na wengine asilimia 20 ya hisa za kampuni hiyo .
Didi Chuxing inasema kuwa inatoa safari milioni 14 kwa siku na inadai kuwa na asilimia 87 katika soko la hisa la China.
Kampuni hiyo inaungwa mkono na kampuni kubwa za mtandao za Tencent na Alibaba,na pia imewekeza katika kampuni pinzani ya Uber huko Marekani Lyft